Uhalisia wa mambo ni kwamba suruwali kwa mwanamke ni katika wahyi wa Shaytwaan. Vinginevyo wanachuoni wote wakubwa wa nchi hii wamefutu juu ya uharamu. Mzungumzaji, ambaye ni mimi, nimefutu juu ya kwamba ni haramu. Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) amefutu kwamba ni haramu. al-Lajnah ad-Daaimah wamefutu juu ya kwamba ni haramu. Shaykh ´Abdullaah bin Jibriyn amefutu juu ya kwamba ni haramu. Hawa ndio vigogo wa wanachuoni wa nchi. Ikiwa watu wa kawaida hawarejei kwa mfano wa watu kama hawa watarudi kwa nani?

Kwa ajili hiyo natilia nguvu kwamba ni wajibu kumkataza mwanamke kuvaa suruwali hata kama ni mbele ya mume wake. Mume wake hana haja ya kuvaliwa suruwali wala ya kumvalia kanzu [za kiume]. Inafaa kwake kulala na mume wake juu ya kitanda bila mtupu. Suruwali ya nini kama sio Shaytwaan kuwapambia baadhi ya watu mambo mabaya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1593
  • Imechapishwa: 15/03/2020