Shaykh ´Ubayd al-Jaabiriy Kuhusu Mauaji Ya Charlie Hebro


Swali: Kama unavojua jumatano tarehe 07-01-2015 wameuawa watu kumi na mbili ambapo wanane ni waandishi wa khabari na polisi mmoja katika makao makuu ya gazeti mjini Paris. Waliofanya tendo hili la jinai wanadai kuwa ni kulipiza kisasi juu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Leo imekuwa waislamu wote wanaashiriwa kidole. Jana kuna Misikiti iliyoteswa kwa kurushiwa mabomu. Salafiy anatakiwa kuwa na msimamo gani juu ya mambo haya ya kigaidi? Ni zipi nasaha zako kwa waislamu wote nchini Ufaransa na khaswa walinganizi na wahubiri Salafiyyuun?

Jibu: Mosi haya sio katika matendo ya Ahl-us-Sunnah. Bali ni matendo ya waeneza machafuko katika Khawaarij na wenye kufuata mwenendo wao ijapokuwa watakuwa ni wenye kujinasibisha na Uislamu.

Pili ninawaambia majirani zenu makafiri wafaransa na wengine walioko Ulaya na Amerika ya kwamba hawawezi kupata mwanachuoni anayefuata Sunnah mwenye kukubaliana na matendo kama haya na kuyaunga mkono. Ahl-us-Sunnah, kuanzia wanachuoni wao na wanafunzi na mpaka kwa wale wasiokuwa wanafunzi, wanakemea matendo kama haya ya fujo. Walioyafanya aidha ni Khawaarij au wajinga wasiojua Sunnah na wala hawajui namna Ahl-us-Sunnah wanavotangamana na majirani zao wasiokuwa waislamu. Ahl-us-Sunnah ni wenye kutangamana kwa wema na majirani zao na ni wenye kutimiza ahadi. Hawasapoti mambo kama haya ya vurugu na ya kipumbavu.

Kwa kumalizia ninawanasihi wanangu katika waislamu, sawa ikiwa ni wahubiri, waalimu na walinganizi watangaze wazi wazi kujikana kwao na matendo haya ya kipumbavu. Wawape taarifa wachunga amani [kituo cha polisi] na kila yule ambaye wanaweza kumfikia kuhusu haya.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.spfbirmingham.com/
  • Imechapishwa: 13/01/2015