Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh kuhusu Hadiyth-ul-Qudsiy

Kuhusiana na Hadiyth-ul-Qudsiy maana yake kwa njia ya istilahi wanachuoni wametofautiana. Wana maelezo mengi juu ya hilo. Kauli inayoenda sambamba na I´tiqaad ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba, Hadiyth-ul-Qudsiy kwa njia ya matamshi yake inatokana na Allaah (Jalla wa ´Alaa) na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) huipokea kwa matamshi yake na hana haki (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kugeuza matamshi yake.

Wanachuoni wengine wamesema kuwa maana yake inatokana na Allaah (´Azza wa Jall) na matamshi yake yanatokana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo imeruhusiwa kwake kugeuza matamshi yake. Kauli hii haina dalili.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 339
  • Imechapishwa: 14/05/2020