Shaykh Rabiy´ anawalazimu wengine kuwafanyia Tabdiy´ maadui zake

Swali: Ni vipi kumraddi anayesema kwamba Shaykh Rabiy´ anawalazimu wengine kuwafanyia Tabdiy´ maadui zake na kwamba hili halina lolote na Manhaj ya Salaf?

Jibu: Mimi nijuavyo ni kwamba Shaykh Rabiy´ hawalazimu wengine kuwafanyia Tabdiy´maadui zake. Nijualo ni kwamba Shaykh Rabiy´ anatilia umuhimu mkubwa katika kueneza Sunnah na kubainisha Sunnah na kutahadharisha Bid´ah na Ahl-ul-Bid´ah. Akiulizwa au akikaa na wengine katika wanafunzi na ikapelekea kuulizwa juu ya hali ya Ahl-us-Sunnah na hali ya Ahl-ul-Bid´ah na kuwaelezea watu ambao wametumbukia katika Bid´ah, anabainisha hilo kwa dalili. Wakati anapobainisha hilo kwa dalili, anachotaka ni mwanafunzi huyu mwenye ufahamu anaposikia dalili ajitahidi kwa haki na abainishe kwa dalili. Hamlazimishi yeyote kumfuata kichwa mchunga au kufuata kauli yake pasina hoja wala dalili. Hili ndilo nijualo juu ya hali ya Shaykh Rabiy´. Sijui kuwa Shaykh Rabiy´ anawalazimu watu kuwafanyia Tabdiy´ maadui zake. Shaykh Rabiy´ anachowalazimisha watu ni kufuata dalili. Dalili ikisimama na kuonesha kwamba kitendo cha mtu ni Bid´ah na Shaykh akabainisha suala hili kwa mwanafunzi, ni lazima kwa mwanafunzi kufuata dalili hii. La sivyo anakuwa ni mwenye kuacha Kitabu cha Allaah, Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Manhaj ya Salaf.

Pengine aliyesema kuwa Shaykh Rabiy´ anawalazimisha wengine kuwafanyia Tabdiy´ maadui zake, amefahamu kimakosa hali hii. Kwa sababu hatujui kuwa Shaykh Rabiy´ amewajengea uadui watu hawa kwa ajili ya mambo ya kibinafsi au kwa ajili ya maslahi fulani. Tujuavyo ni kwamba Shaykh Rabiy´ amejenga uadui na kutahadharisha kwa mtu ambaye amekwenda kinyume na Qur-aan, Sunnah na Manhaj ya Salaf-us-Swaalih. Hili ndio tunalojua kwa Shaykh Rabiy´ – Allaah Amuhifadhi. Sisemi kwamba amekingwa na madhambi na hakosei. Hata kama anafanya kosa, ni mwanaadamu tu. Hata hivyo ninasema hili ndio linalojua juu ya Shaykh na Allaah ndiye Mwenye kujua zaidi.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin ´Umar Baazmuul
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=135099
  • Imechapishwa: 07/05/2018