Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy kuhusu chuo kikuu cha Kiislamu cha al-Madiynah

Chuo kikuu cha Kiislamu [al-Madiynah] kimeasisiwa kwa lengo kuu na madhumuni matukufu, nayo ni kuwalea wanafunzi wake juu ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa salla) kwa mujibu wa uelewa wa Salaf-us-Swaalih.

Wanachuoni wakubwa ndio wamesimama nyuma ya uanzilishi na wanatoka ndani ya nchi na nje ya nchi. Miongoni mwao anachukua nafasi ya mbele kabisa Muftiy wa Saudi Arabia Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah). Mtu wa kwanza aliyeteuliwa kuwa mudiri wake ni ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah).

Watu kutoka katika ulimwengu mzima walikuja kwenda al-Madiynah. Mimi nilikuwa mmoja katika wale waliosoma hapo. Nilitakharuji hapo na nikafundisha hapo kwa miaka mingi mpaka nilipostafu.

Silebasi yake ni kubwa. Imesimama juu ya Qur-aan na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na lengo lake ni kama nilivyotokea punde kutaja, ni kuwalea wanafunzi wake juu ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa salla) kwa mujibu wa uelewa wa Salaf-us-Swaalih.

Lakini wameichafua baadhi ya Ahl-ul-Bid´ah na Bizbiyyuun. Wanaharibu yale wanayoweza kuyaharibu katika chuo kikuu hicho. Ninamuomba Allaah awafanye wale wahusika waweze kukilinda chuo kikuu hichi dhidi ya watu hawa wanaowaharibu wanafunzi wa chuo kikuu hichi na waliyoko nje yake.

Mimi nahimiza kusoma katika chuo kikuu hichi na ninatahadharisha watu hawa katika al-Ikhwaan al-Muslimuun na wengineo. Wanapokea kazi kutoka nje ya nchi zinazoelekezwa katika chuo kikuu hichi. Kitu cha kwanza wanapotua al-Madiynah, wanaanza kuwatahadharisha wanafunzi dhidi ya wanachuoni wa Saudi Arabia na mfumo wao. Wanawaharibu wale wanaowaweza kuwaharibu na wanasalimika wale wanaoweza kusalimika.

Mimi nawanasihi wanafunzi kusoma ndani yake, lakini natahadharisha dhidi ya watu hawa wenye kuenezwa ufisadi katika ardhi. Mwanafunzi anapofika kutoka nje ya nchi, sawa awe ametoka Ethiopia, Misri au nchi nyingine yoyote, akae chonjo dhidi ya watu sampuli hii punguani na watu waharibifu wanaopiga vita malengo na madhumuni ambayo chuo kikuu kimeasisiwa juu yake. Wanaharibu sana. Tayari nimekwishazungumza ndani ya chuo kikuu na kusema kuwa wanafunzi wengi wanakuja hapana na ´Aqiydah mbovu. Wanamaliza sekondari, chuo kikuu na huenda wakafikia mpaka masomo ya juu. Kisha wanarudi nchi zao wakiwa na ´Aqiydah zao hizi mbovu. Hili ni jambo linalojulikana kati ya wale wahindi ambao ni Ahnaaf na Maaturiydiyyah waliopindukia na wengineo vilevile.

Wako wengine wanaobaki vizuri. Ima katika msingi wao wamekutwa ni Salafiyyuun au wanajifunza Salafiyyah baada ya kusoma katika chuo kikuu cha Kiislamu na kuchuma faida kutoka katika mifumo yale iliyonyooka.

Narudi kusema kwa mara nyingine ya kwamba chuo kikuu cha Kiislamu ni chuo kikuu kizuri. Wanafunzi wanatakiwa kusoma kwenye chuo kikuu hicho na wachukue ´Aqiydah na mfumo wake. Pia vilevile nawanasihi na kutahadharisha na wale wenye kutaka kueneza ufisadi juu ya ardhi wamche Allaah. Wasikiharibu chuo kikuu cha Kiislamu. Hakuna kitu Ummah wa Kiislamu unahitajia kama mfumo wa Salaf ambao unawakilishwa ikiwa ni pamoja vilevile na chuo kikuu hichi cha Kiislamu. Kinawalea wanafunzi juu ya Qur-aan na Sunnah na kinawaepusha na misimamo ya kupetuka inapokuja katika madhehebu na I´tiqaad. Kinafunza juu ya misingi hii.

Yule ambaye Allaah anamtakia kheri asome katika chuo kikuu hichi na atakharuji hapo akiwa na ´Aqiydah na mfumo wake. Baada ya hapo arudi katika mji wake na kueneza Sunnah na masomo yake.

Atakayeninasibishia mimi mengine mbali na haya, amenisemea uongo na kunizulia.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=4575
  • Imechapishwa: 22/01/2017