Tazameni enyi ndugu! Ndugu huyu ni mgonjwa! Asinukuu kutoka kwangu kitu chochote, ni uongo na batili. Simuamini na wala simruhusu anukuu kutoka kwangu neno hata moja. Chochote ambacho atanukuu kutoka kwangu juu ya fulani na fulani, na khaswa Tabdiy´, mimi niko mbali na ayasemayo. Kuwa ni mwenye adabu, kijana! Kama unataka kutafuta elimu nenda kwanza Hospitali ujitibishe kisha ndio uje. Lakini kuwa mgonjwa kisha unanukuu kutoka kwangu vitu na kuharibu Da´wah? Mche Allaah! Huyu ni muharibifu. Mche Allaah! Kisha baadae unawafanyia Tabdiy´ Salafiyyuun na unawatuhumu kwa Bid´ah. Mche Allaah, ewe ndugu yangu!

Kijana: Nani?

al-Madkhaliy: Wewe. Unamfanyia Tabdiy´ huyu na yule. Unawafanyia Tabdiy´ watu bora katika Salafiyuun?

Kijana: Ni Ikhwaaniy, Shaykh!

al-Madkhaliy: Ikhwaaniy? Nani mwenye kukusadikisha? al-Ikhwaan wanakaa kwangu?

Kijana: Wewe huwajui.

al-Madkhaliy: Hapana, sio al-Ikhwaan. Wewe ndiye Ikhwaaniy.

Kijana: Wewe huwajui.

al-Madkhaliy: Wewe ndiye Ikhwaaniy. Wao kamwe sio al-Ikhwaan.

Kijana: Hawamfanyii Tabdiy´ Bakr Abu Zayd.

al-Madkhaliy: Hata na mimi.

Kijana: Nini?

al-Madkhaliy: Bakr Abu Zayd simfanyii Tabdiy´. Mtu amekuwa mzushi ikiwa hakumfanyia Tabdiy´ Bakr Abu Zayd? Huu ndio mfumo wa Salaf?

Kijana: Anza kusoma kitabu chako.

al-Madkhaliy: Acha, wewe mwanangu!

Kijana: Wewe haumfanyii Tabdiy´ Bakr Abu Zayd?

al-Madkhaliy: Usimfanyii Tabdiy´ Bakr Abu Zayd wala usimwongelee mtu yeyote! Maneno yake hayakubaliwi.

Kijana: Umemsikia ametubia, Shaykh?

al-Madkhaliy: Mche Allaah!

Kijana: Umemsikia ametubia, Shaykh?

al-Madkhaliy: Sikumfanyia Tabdiy´. Alikosea.

Kijana: Nini?

al-Madkhaliy: Sikumfanyia Tabdiy´. Alifanya kosa na pengine alitubia… Nyote mkono hapa. Mkisikia lolote, basi jueni kuwa ni muongo. Mmesikia? Nyote mnukuu hili kutoka kwangu. Nyote mnukuu hili kutoka kwangu. Mwenye kunukuu kutoka kwangu ya kwamba nimefanyia Tabdiy´ Bakr Abu Zayd, basi ni muongo. Mimi ndiye nilikuwa na mzozo na yeye. Nilimradi na kubainisha haki bila ya kumfanyia Tabdiy´. Watu walitaka nimfanyie Tabdiy´ Safar na Salmaan. Nikakataa. Waache wanachuoni wahukumu wao. Wakati huo kulikuwepo wanachuoni wakubwa kama Ibn Baaz na Ibn ´Uthaymiyn. Kwa ajili ya adabu niliwaacha waanchuoni wahukumu wao. Huyu mwendawazimu anaenda huku na kule na kuwafanyia Tabdiy´ watu kwa jina la Salafiyyah. Kisha baadae anasema kuwa mimi nimemsema ash-Shuraym vibaya. Ninaapa ya kwamba ni muongo. Hakusikia neno hata moja kutoka kwangu si kuhusu ash-Shuraym, as-Sudayas wala mtu mwingine. Baadhi ya watu wanadhuru Salafiyyah kwa jina la Da´wah. Wanadhuru Da´wah ya Salafiyyah. Hawaongei kwa elimu, adabu au kitu. Wanaropokwa-ropokwa mpaka maadui wanashinda kwa kitu kisichojulikana.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=yx572V23naY
  • Imechapishwa: 07/05/2018