Shaykh Ibn Baaz anaona ulazima wa kulala na nia katika funga ya Shawwaal?

Swali: Je, ni kweli kwamba Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) anaona kuwa ni lazima mtu kulala na nia usiku katika funga ya siku sita za Shawwaal?

Jibu: Si kweli. Hali hiyo inakuwa katika funga ya lazima. Ikiwa hakulala na nia na akafunga mchana funga yake inasihi. Siku sita za Shawwaal zote zimependekezwa. Hali hiyo inakuwa katika funga ya lazima. Yule ambaye hakulala na nia sehemu ya usiku basi funga yake haisihi. Inahusu swawm ya lazima. Vivyo hivo inahusu funga ya kulipa deni la Ramadhaan, nadhiri na kafara. Kuhusu swawm iliyopendekezwa jambo lake ni pana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 31/10/2020