Shaykh amesema kuwa masuala ya uasi kwa kiongozi yana tofauti

Swali: Kuna mtu yuko na hoja tata kuhusu kumfanyia uasi kiongozi. Amemsikia Shaykh aliyesema kuwa masuala hayo yana tofauti tangu hapo kale na akataja msimamo wa az-Zubayr dhidi ya al-Hajjaaj na vivyo hivyo al-Husayn [dhidi ya Yaziyd bin Mu´aawiyah]. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Mosi ni kwamba dalili ya kikweli inapatikana ndani ya Qur-aan na Sunnah. Akipatikana mtu ambaye amefanya kitendo na akakosea, haijalishi kitu ni nani, basi kosa lake halizingatiwi kuwa ni dalili dhidi ya Uislamu. Wakati alipofariki Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) Yaziyd ndiye ambaye alichukua uongozi. Hakutenda kwa mujibu wa ukhaliyfah kwa miaka thelathini na kisha baada ya hapo ukafuatiwa na utawala wa ufalme.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Haqiyqat-ul-Bay´ah fiyl-Islaam wa Bayaan Shuruutwihaa wa Khatwar Naz´ihaa http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148858
  • Imechapishwa: 18/12/2020