Shaykh al-´Adaniy kuhusu ad-Duwaysh, al-Qarniy, al-´Awdah na ash-Shanqiytwiy

Swali: Vipi hali ya watu hawa na je inatakiwa kusikiliza mikanda yao; Ibraahiym ad-Duwaysh, ´Aaidh al-Qarniy, Salmaan al-´Awdah na Muhammad al-Mukhtaar ash-Shanqiytwiy?

Jibu: Nijualo kuhusu watu hawa ni kwamba hawafuati njia yetu na Da´wah yetu. Ibraahiym ad-Duwaysh, ´Aaidh al-Qarniy, Salmaan al-´Awdah na Muhammad al-Mukhtaar ash-Shanqiytwiy ni katika vigogo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Tumesikia kuwa ash-Shanqiytwiy pia anafuata njia moja kama wao, hata kama atakuwa ni khafifu kuliko wao. Hawa ni katika viongozi na khaswa Salmaan al-´Awdah, ad-Duwaysh na al-Qarniy. Kadhalika ash-Shanqiytwiy ambaye analingania katika Da´wah yao na ana Taswawwuf na baadhi ya ukhuurafi.

Kwa ajili hii sisi tunawanasihi kutosheka na vitabu na mikanda ya Ahl-us-Sunnah. Kuna kheri ambayo – in shaa Allaah – iliosafi. Na khaswa wanachuoni waliobobea katika elimu. Hii ndio nasaha ya Ahl-us-Sunnah. Baadhi yao wamepiga mfano; ni jambo linaloingia akilini wewe uko na chanzo cha maji masafi kabisa na badala yake unakunywa kutoka kwenye chanzo cha maji machafu? Hali kadhalika inaweza kusemwa kuhusu mikanda na vitabu vya Ahl-us-Sunnah. Humo kuna bayana, kheri na mawaidha yote wakati uko na uhakika na Dini yako na Manhaj yako. Tofauti na mikanda ya watu hawa. Watu wengi wanadai kuwa ndani yake wanaguswa kwenye nyoyo zao, mawaidha na baadhi ya faida. Hata kama unapata kitu katika faida, unaweza kuathirika kwa madhara mengine pasina wewe kujua. Mtu akiwasikiliza sana moyo unaambatana nao. Shaytwaan anampambia yale wanayokuja nayo. Ukisikiliza mikandah hii kuhusu kuhifadhi Swalah na mkanda wa pili kuhusu kuwatendea wema wazazi na mkanda wa tatu kuhusu Tawhiyd na mkanda wa nne kuhusu kujiepusha na madhambi na maasi, moyo utaambatana na muongeaji huu. Kisha baadaye watie sumu zao katika mikanda yao na vitabu vyao. Ni Ahl-us-Sunnah wangapi wamepotea kwa sababu ya kusikiliza watu hawa. Mtu anadhoofika siku baada ya siku na anaanza kuona kuwa hawa wako juu ya msitari, wapigana Jihaad na kadhaa na kadhaa. Hakuna kitu kama kuwa na moyo uliosalimika.

Kitu ninachowanasihi watu wote ni kutosheka na kusikiliza mikanda ya Ahl-us-Sunnah ambao wanaaminika kwa elimu na Manhaj yao na khaswa wanachuoni waliobobea katika elimu. Utapata mawaidha yanayoongelea Kasema Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na faida za kielimu na zenye faida na kunufaika na Manhaj ya wazi kabisa, salama na ilionyooka. Tunatahadharisha ndugu zetu kusikiliza au kusoma katika vitabu vya watu hawa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema katika Kitabu Chake Kitukufu:

“Na unapowaona wale wanaoyaingilia mazungumzo Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka watumbukie katika mazungumzo mengineyo.” (6:68)

“Naye amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo.” (04:14)

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin ´Umar al-´Adaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1932&PageN
  • Imechapishwa: 28/07/2020