Sharti Ya Salafiyyah Kumtembelea Rabiy´ al-Madkhaliy?


Swali: Baadhi ya watu wanasema sio miongoni mwa masharti ya Salafiyyah kumtembelea Shaykh Rabiy´. Kwa ajili hiyo wanaacha kuwatembelea Mashaykh wa Salafiyyah.

Jibu: Nitatoa jibu la jumla kuhusiana na hili na mengine. Miongoni mwa alama za Ahl-us-Sunnah ni kuwapenda Ahl-us-Sunnah. Alama ya Sunniy ni kuwapenda Ahl-us-Sunnah. al-Asma´iy amesema:

“Wakati nyoyo zinapokutana basi hukaribiana kama jinsi miili inavosuhubiana.”

Ikiwa unampenda mtu basi ni lazima utilie bidii kukutana naye. Ibara hii sisi tunaijua tangu muda mrefu. Lengo ni kuwatukana Mashaykh wa Salafiyyah na khaswa Shaykh Rabiy´. Haliwadhuru Mashaykh wa Salafiyyah wala Shaykh Rabiy´. Akiwatembelea, ninamuombea Du´aa. Analipwa ujira kwa hilo. Akiacha kuwatembelea hawapungukiwi na kitu wala kudhurika na hilo.”[1]

————

(1) Imaam adh-Dhahabiy amesema:

“Kuna mtu katika watu wa ´Abdullaah bin Munayyir alienda Bukhaaraa kwa sababu ya haja. Wakati aliporudi Ibn Munayyir akamwambia: “Ulikutana na Abu ´Abdillaah [al-Bukhaariy]?” Mtu yule akasema: “Hapana.” Hivyo akawa amemtimua na kusema: “Hakuna kheri yoyote kwako ikiwa umefika Bukhaaraa na kuacha kukutana na Muhammad bin Ismaa´iyl [al-Bukhaariy].” (Siyaar A´laam-in-Nubalaa´ (12/424))

Imaam Abu Daawuud amesema:

“Watu wengi walienda kuhiji wakiwa na uchangamfu kwa ajili ya kukutana na ´Uyaynah. Walisongamana kwa kumzunguka katika yale masiku ya Hajj.” (Tabaqaat-ul-Mufassiriyn (01/197))

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/3478
  • Imechapishwa: 03/12/2014