Swali: Ni zipi sharti za kuoa wanawake wa Ahl-ul-Kitaab?

Jibu: Awe ni mwema mwenye kujichunga na machafu:

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ

“… na chakula cha wale ambao walipewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao na [mmehalalishwa kuwaoa] wanawake wenye kujichunga na machafu miongoni mwa waumini wanawake na wanawake wenye kujichunga na machafu miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu.” (05:05)

Wanawake wenye kujichunga (الْمُحْصَنَاتُ) bi maana waliotakasika na uzinzi. Mwanamke wa kitabu imeshurutishwa kwake awe ametakasika na zinaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12934
  • Imechapishwa: 20/09/2020