66- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Akiwahi mmoja wenu Sajdah moja ya swalah ya ´Aswr kabla ya jua kuzama basi aikamilishe swalah yake. Na akiwahi Sajdah ya moja ya swalah ya Subh kabla ya jua kuchomoza basi aikamilishe swalah yake.”[1]

Faida ya pili: Hadiyth inawaraddi wale wanaosema kuwa inawahiwa kwa kuwahi sehemu yoyote ile ya swalah (ijapo Takbiyrat-ul-Ihraam), basi mtu anakuwa ameiwahi swalah. Haya yanakwenda kinyume na udhahiri wa Hadiyth. Mtunzi wa kitabu “Manaar-us-Sabiyl” ameyanasibisha haya kuwa ni moja katika maoni ya ash-Shaafi´iy. Hata hivyo ni mtazamo katika madhehebu yake, kama ilivyotajwa katika “al-Majmuu´”[2] na an-Nawawiy. Maoni haya pia ndio ya Hanaabilah licha ya kuwa imenukuliwa kuwa Imaam Ahmad amesema:

“Swalah haidirikiwi isipokuwa kwa Rak´ah moja.”

Yeye ndiye ana haki zaidi ya Hadiyth hii na Allaah ndiye anajua zaidi.

´Abdullaah bin Ahmad amesema:

“Nilimuuliza baba yangu kuhusu bwana mmoja anayeswali swalah ya alfajiri na wakati alipoinuka katika Rak´ah ya pili jua likachomoza. Akajibu: “Aikamilishe swalah yake. Inafaa.” Nikasema kumwambia baba yangu: “Unasemaje juu ya ambaye anasema kuwa swalah hiyo haisihi?” Akajibu: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya swalah ya asubuhi kabla ya jua kuchomoza basi ameiwahi.”[3]

[1] al-Bukhaariy (1/148), an-Nasaa’iy (1/90), al-Bayhaqiy (1/368) na as-Sarraaj (1/59).

[2] 3/63.

[3] Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 46.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/138-139)
  • Imechapishwa: 19/04/2020