Sharti wakati wa kunakili fatwa za wanazuoni na utabiri wa hali ya hewa

Swali: Punde kidogo nimesikia kwenye redio kwamba kutakuwa na dhoruba ya theluthi siku ya alkhamisi. Je, mimi kama muislamu (na si kama mtaalam wa hali ya hewa) kutangaza utabiri huo?

Jibu: Je, inafaa kwako kusema kwamba Shaykh al-Albaaniy kwa mfano anasema kuwa kuvuta sigara ni haramu?

Muulizaji: Inafaa.

al-Albaaniy: Inafaa na haifai. Zingatia tofauti. Ukisema kuwa Shaykh al-Albaaniy anasema hivi, umesema kweli. Lakini ukipatwa na hamasa na ukasema kuwa uvutaji wa sigara ni haramu na pale unapoulizwa utoe dalili, unasema kuwa Shaykh al-Albaaniy ndio amesema hivi. Usifanye hivo. Sema hivo tokea mwanzo.

Kwa hivyo haifai kwako kusema kwamba siku ya alkhamisi kutakuwa namna hii, kwa sababu huna elimu yoyote. Hata hivyo unaweza kusema kwamba mtaalam wa hali ya hewa amesema au kwamba umesikia kwenye redio, umesoma kwenye gazeti na mfano wake. Unatakiwa kunakili kama ulivosoma na hapo utakuwa si mwenye kwenda kinyume na Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1023)
  • Imechapishwa: 02/07/2021