Swali: Ni ipi hukumu mwanamke kutumia dawa za kuzuia mimba au kuzuia hedhi ikiwa mume wake ameridhia kitendo hicho?

Jibu: Inafaa kwa sharti mbili:

1- Kuwepo na haja kama mfano wa kufunga pamoja na wengine katika Ramadhaan, kutetekeleza faradhi ya hajj au watoto wanafuatana kwa haraka. Katika hali hii anatumia tembe hizi kwa ajili ya kupangilia.

2- Visimdhuru katika afya yake na hilo lisipelekee kukata kizazi.

Ama ikiwa anafanya hivo pasi na sababu au kwa sababu ya kutokutaka watoto wengi na badala yake anataka kuzaa mtoto mmoja au wawili peke yake, jambo hilo limekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha na kusema:

“Oeni wanawake wenye mahaba na wenye kuzaa sana. Hakika mimi nitajifakharisha mbele ya ummah zengine siku ya Qiyaamah.”

Waislamu wameamrishwa kukithirisha Ummah, kuhakikisha kujifakharisha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuzaa watoto wengi watakaomuabudu Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 06/01/2019