Sharti kwa mwanamke kuhudhuria darsa msikitini

Swali 1346: Je, inajuzu kwa dada wa Kiislamu kuhudhuria vikao vya elimu na darsa za ki-Fiqh msikitini?

Jibu: Ndio. Inafaa kwa mwanamke kuhudhuria vikao vya elimu. Ni mamoja somo hilo linahusu hukumu za Fiqh au hukumu za ´Aqiydah na Tawhiyd. Kwa sharti asiwe ni mwenye kujitia manukato wala kuonyesha mapambo. Vilevile ni lazima awe mbali na wanaume na asichanganyike nao. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safu bora za wanawake ni zile za nyuma na ovu ni zile za mbele.”

Hayo ni kwa sababu zile za mbele zinakuwa karibu zaidi na wanaume kuliko zile za mbele yake. Hivyo za nyuma zikawa ni bora kuliko za mbele.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 547
  • Imechapishwa: 20/08/2019