Shahaadah upya baada ya kukufuru

Swali: Mwenye kuchezea shere kitu katika Shari´ah za Uislamu kisha akatubu ni lazima atamke shahaadah mbili?

Jibu: Akitubu basi itambulike kuwa tawbah inafuta yaliyo kabla yake.

Swali: Atalazimika kutamka shahaadah mbili ili afanye upya Uislamu wake?

Jibu: Hapana, si lazima. Itatosha akubali kosa lake na atubu. Baadhi ya Fuqahaa´ wanaona kuwa atamke shahaadah mbili. Kwani kufanya hivo ni kukubali kile alichokipinga. Kwa mfano akisema kuwa swalah au swawm sio lazima. Kisha akatubu basi Allaah anamsamehe na inatosha kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 99
  • Imechapishwa: 27/07/2019