Swali: Je, inafaa kwa yeyote kukataza kitu kilichoruhusiwa?

Ibn ´Uthaymiyn: Kivipi?

Swali: Serikali ikamkataza mtu kufungua biashara ambayo imeruhusiwa. Je, atii jambo hilo?

Jibu: Ni lazima kwa mtu kumsikiliza na kumtii mtawala muda wa kuwa sio katika maasi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ni lazima kwa muumini kusikiliza na kutii katika yale anayoyapenda na kuyachukia muda wa kuwa hajaamrishwa maasi. Akiamrishwa maasi basi hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Jengine ni kwamba hii ni sharti katika mkataba; ima utekeleze wajibu wa kazi au uache hiyo kazi. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ

”Enyi walioamini! Timizeni mikataba.”[1]

وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا

”Timizeni ahadi, kwani hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa.”[2]

Ni lazima kwetu sisi kuwatii watawala wetu katika kila kitu muda wa kuwa sio maasi. Wakituamrisha kufanya maasi haifai kuwasikiliza wala kuwatii.

[1] 05:01

[2] 17:34

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (9 B)