Sawa ni al-Madiynah an-Nabawiyyah badala ya al-Madiynah al-Munawwarah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuita mji wa al-Madiynah “al-Madiynah al-Munawwarah”?

Jibu: Jina “al-Madiynah al-Munawwarah” limetangaa kwa watu. Lakini kitu hichi kimetokea baadaye. Vitabu vyote vya kale walikuwa wakisema “al-Madiynah” pekee au wakati mwingine wanasema “al-Madiynah an-Nabawiyyah”. Uhalisia wa mambo ni kwamba al-Madiynah  al-Munawwarah sio jambo la kipekee juu ya mji wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu kila mji ambao Uislamu uliingia ndani yake uliangazwa na Uislamu. Kwa sababu hiyo al-Madiynah an-Nabawiyyah haiwi na sifa ya kipekee ikiwa tutasema “al-Madiynah al-Munawwarah”. Lakini pamoja na haya hatusemi kuwa ni haramu. Bali tunasema kwamba hili ni jina ambalo watu wamezowea. Hivyo hakuna ubaya. Lakini bora ni kusema “al-Madiynah an-Nabawiyyah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1500
  • Imechapishwa: 07/02/2020