Sauti ya mwanamke sio ´Awrah         

Swali: Je, sauti ya mwanamke ni ´Awrah? Hili pamoja na kuwa sauti yake inatofautiana kutegemea na kile anachokitaka.

Jibu: Sauti ya mwanamke sio ´Awrah. Lakini mwanamke amekatazwa asiilegeze sauti yake asije kutamani yule ambaye ndani ya moyo wake mna maradhi. Hii ina maana ya kwamba asiongee maneno laini. Hili linahusu sawa iwe katika maneno yake, katika kule kuyatamka kwake na mfano wa haya. Haya ni haramu. Kuhusu kuongea maneno ya kawaida sio haramu na wala sio ´Awrah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
  • Imechapishwa: 03/05/2020