Saudi Arabia ni nchi ya Kishari´ah iliyosimama juu ya Qur-aan na Sunnah

Swali:  Baadhi ya watu wanaeneza utata juu ya Saudi Arabia kwamba sio nchi ya Kiislamu kwa sababu kumeenea ribaa na Shari´ah haisimamishwi kikamilifu na kwa ajili hiyo anakufurisha. Tunataraji nasaha kutoka kwako.

Jibu: Mtu kama huyu hatakiwi kujibiwa. Anataka tu kurusha tuhuma za kimakosa na kufunika jua katikati ya mchana. Mtu kama huyu asijibiwe. Anafuata matamanio yake. Hatokinaika vovyote utakavyosema.

Nchi imejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah. Ni nchi ya Kishari´ah iliyosimama juu ya Qur-aan na Sunnah. Inahukumu kwa Shari´ah. Sio sharti iwe kikamilifu. Kuna mapungufu[1]. Midhali ´Aqiydah ni sahihi na mfumo umejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah… Hata kama kutapitika baadhi ya vijimakosa na mapungufu.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/vipi-saudi-arabia-ni-nchi-ya-kiislamu-na-kumejaa-maasi/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Imechapishwa: 27/08/2020