Swali: Je, ni sahihi kwamba Khatwiyb anatakiwa kutoa salamu mbili; salamu wakati anapoingia na salamu wakati baada ya kupanda juu ya mimbari?

Jibu: Bali wanasema kuwa anatakiwa kutoa salamu mara tatu. Salamu ya kwanza ni pale anapoingia kwenye mlango; anawasalimia wale walioko pale. Salamu ya pili ni pale anapofika kwenye mimbari; anawasalimia wale walioko pale. Salamu ya tatu ni pale anapopanda kwenye mimbari. Je, ni jambo linalomdhuru? Ni kheri zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/de
  • Imechapishwa: 20/10/2017