Salama zaidi kwa mtu huyu asikusanye wala kufupisha swalah


Swali: Mimi nafunza katika masomo yaliyo mbali na ´Unayzah kwa 115 km. Je, inajuzu kwangu kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr?

Jibu: Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa safari mpaka wake ni yale masafa. Midhali mtu anaenda 83 km basi hiyo inahesabika ni safari. Haijalishi kitu ijapokuwa mtu atarudi ndani ya saa moja. Wanachuoni wengine wanaona kuwa safari ni ile inayozingatiwa na watu kama ni safari. Mfano wa mtu kama huyu ambaye anafunza na kurudi siku hiyohiyo hazingatiwi katika desturi za watu kama ni msafiri. Lililo salama zaidi kwa mtu huyu asikusanye wala asifupishe swalah. Hilo linatakasa zaidi dhimma na kuondosha utata.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (44) http://binothaimeen.net/content/1021
  • Imechapishwa: 21/02/2019