”Salafiyyuun Wanachojua Tu Ni Kujeruhi”


Swali: al-Ahdal anasema kuwa mfumo wa Salafiyyuun una kujeruhi tu na hakuna kusifu. Je, ni kweli?

Jibu: Himdi zote ni Zake Allaah kwa kuwa tunawasifu wanachuoni na kuwaita watu kwenda kwao. Mfano wa hao ni Shaykh Badiy´-´ud-Diyn as-Sindiy, Shaykh al-Albaaniy, ndugu ambao ni wajuzi wa mafundisho ya Hadiyth kama ‘Abdullaah bin Sa´d na Sa´d bin ‘Abdillaah bin Humayd, Shaykh Rabiy’ na Shaykh Ibn Baaz. Hushauri daima katika vitabu vyangu kukaa pamoja nao na kufaidika kutoka kwao na vitabu vyao.

Na kama anamaanisha kuwa msimamo wetu kwa Ahl-ul-Bid´ah uko katika sampuli ya kujeruhi, ni kweli. Wao ndio wameanza:

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا عَلِيمًا

“Allaah Hapendi kutajwa hadharani uovu katika kauli isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa. Na Allaah ni Samiy’an-‘Aliymaa (Mwenye kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).” (04:148)

Wao ndio wameanza. Wakati mwingine wanasema kuwa sisi ni Jamaaat-ut-Takfiyr, wakati mwingine wanasema kuwa sisi ni wagumu, wakati mwingine wanasema kuwa hatuelewi mambo ya kisasa, wakati mwingine wanasema kuwa sisi tunachojua tu ni “ametueleza, ametueleza”. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati watu wawili wanapogombana yule aliyeanza ndio anapata madhambi maadamu mkandamizwaji havuki mipaka.”

Tunaihami tu Sunnah. Hatujihami sisi wenyewe. Tunasikia jinsi wengi wanavyotutukana bila ya kuwarudi. Wale wa Sa’dah waliandika kitabu kiitwacho “Faslul-ul-Khitwaab fiyr-Radd ‘alal-Muftariy al-Kadhdhab”. Wanakusudia mimi. Pamoja na hivyo sikuwarudi. Sintowarudi hata wakifa. Sina muda wa kujitetea mwenyewe. Hata hivyo tunatetea Sunnah hata kama tutahitajia kuiuma na magego. Hatumwachi yeyote kuisema vibaya Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijalishi ikiwa ni Shiy´iy, Suufiy au Ikhwaaniy anayefanya hivo. Tunazitoa nafsi zetu na heshima yetu kwa ajili ya Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 22/04/2015