Salafiyyuun peke yao ndio wanafata Qur-aan na Sunnah katika kila kitu


Kutokana na yale tuliyojifunza na kuona katika yale makundi ya leo yaliopo ulimwenguni, hatumuoni ambaye anajaribu kuisogelea Qur-aan na Sunnah isipokuwa wale wanaojiita Ahl-ul-Hadiyth, Answaar-us-Sunnah katika baadhi ya miji, Salafiyyuun katika miji mingine, Ahl-ul-Hadiyth katika miji mingine na kadhalika.

Kuhusu wale wanaojinasibisha katika makundi mengine, hawajengei hoja kwa Qur-aan na Sunnah katika nyanja zote zinazohusiana na maisha yao binafsi, maisha yao ya jumla, fikira zao, siasa na mengineyo. Hatuwaoni wale ambao daima hutilia mkazo Qur-aan na Sunnah isipokuwa tu kutamka neno:

“Tunafata Qur-aan na Sunnah.”

Kila mmoja anasema hivo, lakini tupeni dalili yenye kuonyesha kuwa mnafata Qur-aan na Sunnah. Hutopata jawabu lolote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (1)
  • Imechapishwa: 19/06/2021