Salafiyyuun Ndio Wanaopambana Na Ugaidi


Yemen Times:

Kunaenezwa tuhuma kwamba Salafiyyuun ni chama cha kigaidi pamoja na kuwa sisi tunajua kuwa ni kundi la Kiislamu na la salama na malengo yake ni kueneza elimu na harakati zinazofanywa na baadhi ya mitiririko ya Kiislamu, kama harakati za Jihaad na mengineyo, hazina msingi na kwamba inahusiana na kuwa na ufahamu mbaya. Tunapenda kujua ni vituo vya kielimu vipi na vingapi vya Ahl-us-Sunnah, au Salafiyyuun, ambavyo wewe unavisimamia.

Jibu: Kuhusiana na vituo, kila ndugu anasimamia kituo chake. Mfumo wetu ni mmoja na unahusiana na kufundisha Qur-aan na Sunnah. Haya wanayajua watawala. Wakati [waziri wa kwanza] ´Abdul-Khariym al-Iryaaniy alipopata simu kutoka, nadhani kutoka London, akaambiwa kuwa kuna kundi lenye msimamo mkali Sa´dah. Akamwambia si kweli na kuwa kuna mwanachuoni tu ambaye anafundisha Qur-aan na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwelezwaji sio kama mwenye kujionea.”

Mshairi amesema:

Hutonifuata ujionee uliyoelezwa?

Anayeona sio kama yule mwenye kusikia.

Da´wah yetu ni kutoka katika Kitabu cha Allaah na kwenda katika Kitabu cha Allaah na kutoka katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwenda katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mimi binafsi nina mikanda mingi ambapo nimewaraddi watu wa malipuaji. Zinahusu pia hata kama hayapitiki Yemen. Kwa sababu yanawatia khofu wananchi na yanaharibu uhusiano baina ya watu na nchi. Ahl-us-Sunnah wanakataza ugaidi. Maadui wa Uislamu ndio ambao wanatakiwa kushtuliwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ameamrisha kuwashtua:

وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّـهِ وَعَدُوَّكُمْ

“Na waandalieni nguvu (silaha) zozote mziwezazo na farasi wa vita (waliofungwa tayari tayari) muwaogopeshe kwayo maadui wa Allaah na maadui zenu.” (08:60)

Kuhusiana na Waislamu, sio halali kwa Muislamu kumshtua Muislamu mwenzake seuze tusiseme kumuua. al-Bukhaariy amepokea katika ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Ibn ´Umar ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Muumini hatoacha kupata uwezo wa kufanya matendo mazuri katika Dini yake mpaka pale atapomwaga damu iliyoharamishwa.”

Ahl-us-Sunnah ndio ambao wanapambana na ugaidi. Lakini tatizo ni kwamba wengine hawasomi vitabu vya Ahl-us-Sunnah na wala hawataki hata kuvisoma. Badala yake wanawasemea uongo kwa mambo wasiyokuwa nayo. Kuna takriban zaidi ya wanafunzi 100.000 ambao wamekuja Dammaaj na kurejea [makwao]. Wote wanajua Da´wah ya Ahl-us-Sunnah na kwamba ni Da´wah inayolingania katika Qur-aan na Sunnah. Watu hawa hawatudhuru sisi. Wanajidhuru wao wenyewe tu. Kuhusu sisi, Da´wah yetu inajulikana. Inajulikana hata kwa watawala.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=40