Swali: Je, kuna Salafiyyah ya zamani na Salafiyyah mpya au kuna Salafiyyah moja tu?

Jibu: Salafiyyah ni moja. Anayedai kuwa kuna Salafiyyah ya zamani na mpya amesema uongo.

Lau tutatazama juu ya ´Aqiydah ya Salaf, kuanzia Maswahabah mpaka hivi leo, tutaona kuwa ´Aqidah ni moja. Haitofautiani kamwe, hata kama watatofautiana katika mambo madogo madogo ambayo sio katika misingi na ´Aqiydah. Wanatofautiana katika mambo madogo madogo, lakini hawahukumiani (hawa kuwahukumu wale). Hii ndio njia ya Maswahabah. Na kuhusiana na ´Aqiydah, Manhaj yao ni moja na ni ile ile kutokea wakati wa Maswahabah mpaka hivi leo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jalliyyah, uk. 9
  • Imechapishwa: 14/07/2020