Swali: Je, Salafiyyah ni kikundi katika vikundi?

Jibu: Mimi nimekwishajibu swali kama hili kwenye makala ndefu iliyosambazwa kwenye gazeti la “al-Muslimuun”. Salafiyyuun ndio walio katika haki. Kujinasibisha na mfumo wa Salaf ni utukufu. Kuifuata na kuyashika kwa magego ni jambo la wajibu. Ni jambo kaliwajibisha Allaah (´Azza wa Jall):

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ

“Kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni.”[1]

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, basi Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!”[2]

Mfumo wa Salaf si jengine isipokuwa ni kufuata njia ya waumini katika Maswahabah, Taabi´uun na as-Salaf as-Swaalih. Dalili ya niliyokwambieni zinapatikana katika marejeo ya kale na ya sasa.

Sio kipote. Lengo la mapote potofu yanataka kuchafua mfumo wa Salaf na kuwazuia watu nayo. Wanasema kwamba sisi ni vyama na wao ni vyama mfano wetu. Salafiyyuun wanasaidiana katika wema na uchaji, jambo ambalo kaliamrisha Allaah. Hakuna Mtume yeyote yule isipokuwa alikuwa akilingania, watu wakimkusanyikia mpaka wanakuwa pamoja kikundi. Hakuna manufaa isipokuwa watu wanakusanyika juu yake mpaka wanakuwa kikundi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilingania na watu wakakusanyika juu yake mpaka wakawa kikundi kinachopambana, kueneza Uislamu na kupigana vita katika njia ya Allaah. Amesema  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waumini ni kama jengo moja; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”

Kwa hivyo ni wajibu kwa kila ambaye anaamini Salafiyyah asimame upande wa nduguye hali ya kumnusuru. Haijalishi kitu hata kama makhaini hawa watawaita kuwa ni “kipote”. Haidhuru kitu. Kwa sababu wao ni kikundi cha Allaah. Lakini je, ni kama mnavofanya nyinyi ambapo mnawaabudu, mnawatakasa wanachuoni wenu na mko tayari kupenda na kuchukia kwa ajili yao? Hapana. Je, wao wameshikamana na wanatetea batili? Hapana. Hili halifai.

Akikosea Ibn Taymiyyah tunasema kuwa amekosea. Akikosea Ibn Baaz tunasema kuwa amekosea. Akikosea Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab tunasema kuwa amekosea. Kweli si kweli? Makosa ya watu hawa ni katika jinsia ya makosa ya maimamu; wakipatia wanapata ujira mara mbili na wakikosea wanapata ujira mara moja. Lakini hatuwezi kufuata kosa lao au kutetea kosa hilo. Tofauti na wanavofanya wao. Wanatetea upotevu mkubwa na wanaona kuwa ni haki.

Tulipoandika kuhusu Sayyid Qutwub ambaye anawatukana Maswahabah, anawakufurisha baadhi ya Banuu Umayyah, dola ya ´Abbaasiyyah, Umawiyyah, anaukufurisha Ummah mzima, anaona kuwa Qur-aan imeumbwa, ana imani ya kwamba Allaah amekita kwenye kila kiumbe na kwamba kila kiumbe ni Allaah, madhehebu ya Raafidhwah, Khawaarij na Bid´ah za zamani na za sasa za kutokea mashariki na magharibi. Pamoja na haya yote ninaapa kwa jina la Allaah wanamtetea, wanapenda na kuchukia kwa ajili yake, wanatetea vitabu vyake, wanapiga vita vitabu ambavyo vinatokana na mfumo wa Salaf. Wanaupiga vita vibaya sana mfumo huu. Je, mmekwishamsikia Salafiy anatetea kosa la fulani na la fulani? Ninaapa kwa Allaah kwamba anakosea fulani husema kwamba amekosea. Ni watu ambao wanakosoana wao kwa wao.

Huyu hapa Hamuud at-Tuwayjiriy amemraddi al-Albaaniy na al-Albaaniy amemraddi  Hamuud at-Tuwayjiriy. Ismaa´iyl al-Answaariy amemraddi al-Albaaniy na al-Albaaniy amemraddi Ismaa´iyl al-Answaariy. Bado ni ndugu japokuwa ni wenye kuraddiana wao kwa wao. ad-Daaraqutwniy, Abu Haatim na Abu Zur´ah walimraddi al-Bukhaariy. Lakini upande wa pili ole wako ukikosoa. Ni Ahl-udh-Dhwalaal. Jambo la kukosoa ni haramu kwao. Haijuzu kukosoa kabisa. Baada ya yote haya wanaulizia mbona sisi hatuna haki sawa (Muwaazanah). Ninaapa kwa Allaah kwamba wao hawana jambo la haki sawa pamoja na kuwa ni yenyewe ni batili. Wameanzisha mfumo wa haki sawa kwa ajili waweze kuwazuia watu kutokamana na njia ya Allaah na waweze kutetea Bid´ah na upotevu. Mazuri yao yako vipi? Mtu wao anafanya Bid´ah mia kubwakubwa kisha ukimkosoa wanakuuliza mbona hukutaja mazuri yake pia? Ni kina nani Murji-ah waliopindukia? Hivi sasa wamejifunza kupitia mambo yanayoendelea Afghanistan na Uturuki. Murji-ah walipindukia wao wenyewe wanashtushwa na mfumo kama huu. Kisha inapokuja juu ya mfumo wa Salaf wanasema kuwa ni Khawaarij makafiri. Ummah umepewa mtihani na ni wenye kukereka na watu, mapote na makundi kama haya.

Salafiyyuun ni kundi la Allaah[3]. Ikiwa italazimika kuwaita ´kundi` basi ni kundi la Allaah. Allaah amesema kuhusu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Zindukeni! Hakika kundi la Allaah ndilo lenye kufaulu.”[4]

[1] 06:153

[2] 04:115

[3] Tazama Salafiyyah ni kundi la Allaah – al-Firqah an-Naajiyah (firqatunnajia.com)

[4] 58:22

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda: al-Akhdh bil-Kitaab was-Sunnah http://www.rabee.net/ar/questions.php?cat=27&id=67
  • Imechapishwa: 11/01/2019