Swali: Nilikuwa naomba tafsiri ya neno “Salaf” na ni kina nani “Salafiyyuun”?

Jibu: Salaf ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao ndio wenye kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) miongoni mwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na wenye kufuata uongofu wao mpaka siku ya Qiyaamah. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa juu ya kundi lililookoka akasema:

“Ni lile lenye kufuata yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/164)
  • Imechapishwa: 23/08/2020