Huenda unajua kuwa hapa kuna uchaguzi. Kwa ajili hiyo nimeulizwa maswali mengi kuhusu uchaguzi na wagombea wa kiislamu waliyoko huko. Tangu hapo mwanzo nilikuwa nikijibu jawabu hili na bado ningali ni mwenye kukinai mpaka hii leo muislamu asiingie bungeni. Ni jambo linalojulikana ya kwamba hakuhukumiwi kwa Shari´ah ya Allaah kwa jumla na jengine ni kwamba wanalazimishwa kula viapo juu ya kuwasapoti baadhi ya watu au nidhamu isiyokuwa ya Kiislamu.

Natambua kwa wengi wenye kuamini Salafiyyah ambao wanaonelea kuwa hakuna tatizo kuingia bungeni. Ni kana kwamba wanaonelea kanuni inayosema “lengo inatakasa njia”. Hii sio kanuni ya Kiislamu. Hata kama bunge hizi zimezungukwa na madhambi mengi wanadai kuwa ni lazima kwao kuingia ndani yake kwa sababu waweze kuboresha mazingara katika bunge. Pindi ninapoulizwa husema kuwa simshauri muislamu kabisa kuwa mgombea katika bunge hizi. Badala ya yeye kutengeneza ataharibika kwa sababu ya wale wengi ambao hawezi kukabiliana nao kwa sababu wao wana nguvu zaidi kuliko yeye.

Lakini upande mwingine kukiwepo waislamu wasiokubali nasaha hizi na wakagombea, hivyo naonelea kuwa hakuna neno mtu akawapigia kura ili kuyaepuka madhara makubwa. Hata hivyo sipendi wakawa kama masomo ya majaribio ya wanyama na wakajiweka wenyewe katika mtihani. Wengi wao wameshajaribu bunge. Syria tangu hapo zamani tuna Dr. Suhayl, Muhammad al-Mubaarak na wengineo. Hapa hata Hizb-ut-Tahriyr wamejiingiza. Miaka kadhaa iliyopita wamemchagua mmoja katika chama chao. Lakini hata hivyo hawakuweza kutengeneza kitu. Msiba huo huo wametumbukia ndani yake ndugu zetu Kuwait.

Maneno yangu yameenea katika nchi nyingi. Nakumbuka kuwa kuna mkanda ambapo niliulizwa swali kama hili pindi nilipokuwa al-Madiynah al-Munawwarah. Mimi naenda kinyume na mwelekeo huu kabisa kabisa. Kwanza ni jambo lisilowezekana kuoanisha kati yake na Salafiyyah kimatendo. Pili mwishowe Salafiyyah inageuka kuwa ni chama iliyofupika kwa watu maalum. Hapo Salafiyyah itatumiwa kwa njia mbili. Njia ya kwanza viongozi watatumia jina la Salafiyyah. Njia ya pili wao wenyewe watakuja kuitumia Salafiyyah ili kuweza kufikia nafasi za juu. Historia ni yenye kujirudi. al-Ikhwaan al-Muslimuun wamekuwa kwa nusu ya karne. Wamejiingiza katika siasa; hakuna si elimu, malezi ya kitabia, wala hakuna kitu. Bado wamesimama pale pale. Wana harakati, lakini bado wamesimama pale pale. Bali huenda wanarudi nyuma. Moja katika madhara ya kujiunga na chama ni kwamba wafuasi wake hujiona. Jambo hilo huwasumbua kutokamana na kile kitendo cha uhakika cha Uislamu na kwa ajili ya Uislamu. Kwa ajili hiyo mimi sikubali kabisa mwelekeo huu uliyochukiliwa na baadhi ya ndugu zetu Salafiyyuun huko Kuwait.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1003)
  • Imechapishwa: 29/01/2017