Salafiy kwa kujifakhari


Swali: Nimjibu vipi mtu ambaye ananiuliza kama mimi ni Salafiy?

Jibu: Ni utukufu. Sema kuwa wewe ni Salafiy kwa fakhari. Jibu rahisi. Ni nini maana ya Salafiy? Salafiy maana yake ni kwamba mimi nawafuata wale waliotangulia katika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wake watukufu na makhaliyfah wake waongofu ambao Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema juu yao:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Wale waliotangulia wa mwanzo [katika Uislamu] miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.”[1]

Lakini usifikirie kuwa kila mtu atakuwa radhi nawe. Kinyanyue kichwa chako na sema kwamba wewe ni Salafiy. Hakuna neno.

[1] 09:100

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Bgo0kcWJihY&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 22/05/2019