Ninawazungumzisha wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah kama vile Shaykh Ibn Baaz na Shaykh al-Albaaniy; uchaguzi ulitajwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakati wa makhaliyfah waongofu, wakati wa Banuu Umayyah au wakati wa Baanuul-´Abbaas? Hayakutajwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala wengineo. Kujengea juu ya hili uchaguzi umetoka kwa maadui wa Uislamu. Haijuzu! Haijuzu!

Salafiyyuun waliyoko Kuwait… Lakini nyinyi mnapiga kura… Masikini nyinyi! Nyinyi mko mbali kabisa na Salafiyyah. Mtu Salafiy Suuniy haingii katika uchaguzi. Kwa kuwa yametujia kutoka kwa maadui wa Uislamu. Ni Twaaghuut!

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا

“Si kwa matamanio yenu wala si matamanio ya Ahl-ul-Kitaab. Atakayefanya uovu atalipwa kwao na wala hatapata badala ya Allaah mlinzi wala mwenye kunusuru.”[1]

[1] 04:123

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yuusuuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 117
  • Imechapishwa: 29/01/2017