Swali: Kuna mwanafunzi mmoja huko Ubelgiji anasoma Jordan na wakati anaporudi Ubelgiji basi anakaa na kushirikiana na Hizbiyyuun. Wanafunzi wake wanachukua elimu kutoka kwa Qutbiyyuun. Hawatahadharishi wanafunzi zake nao. Je, wachukue elimu kutoka kwa mtu huyu?

Jibu: Hapana. Mtu mwenye sifa kama hizi hatakiwi kuwa mwalimu wala mlinganizi. Qutbiyyuun ni Takfiyriyyuun.

Kusema kwamba anakaa nao kwa sababu anawalingania nao, hii ni hoja inayotumiwa na baadhi ya watu kama udhuru. Lakini mwishowe hubainika kuwa yeye ndiye mwenye kuathirika. Mimi natahadharisha mtu kama huyu na mfano wake. Isipokuwa kama itatokea kwa bahati mbaya mtu akajikuta ameingia katika kikao cha jumla na kukatokea mjadala. Vinginevyo Salaf wanasema kwamba Ahl-ul-Bid´ah hawatakiwi kufanywa kama kifaa cha mjadala.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.darulhadith.com/v2/den-som-umgas-med-hizbiyyun-ar-sjalv-en-hizbi/
  • Imechapishwa: 02/12/2018