Salaf, wanawake na familia 9.1


1- Baadhi wamenukuu kwamba Abu ´Aaswim alikuwa na pua kubwa. Akamuoa mwanamke na wakati walipokuwa wamekaa chemba, akamsogelea ili ambusu. Mwanamke yule akasema: “Ondosha goti lako usoni mwangu.” Akasema: “Sio goti. Ni pua.”[1]

2- ´Amr bin ´Aliy al-Fallaas amesema: Nimemsikia Abu ´Aaswim akisema:

“Mama yangu alizaliwa mwaka 110. Mimi nilizaliwa mwaka 122.”[2]

3- Makkiy al-Balkhiy amesema:

“Nimefanya hija mara sitini, nimeoa wanawake sabini, nimeishi karibu na Nyumba kwa miaka kumi na nimeandika kutoka kwa wanafunzi wa Maswahabah kumi na saba. Lau ningelijua kuwa watu watanihitaji basi nisingeandika kutoka kwa yeyote zaidi ya wanafunzi wa Maswahabah peke yao.”[3]

4- Fayyaadhw bin Zuhayr an-Nasaa´iy amesema:

“Tulimuomba mke wa ´Abdur-Razzaaq atuombee ili tupate kumtembelea. Tulipoingia akasema: “Leteni khabari! Mmeomba kunifikia kupitia yule ambaye hulala na mimi juu ya kitanda changu?” Kisha akasoma:

Mwombezi anayekujia hali ya kuwa amevaa shuka ya juu

si kama mwombezi anayekujia hali ya kuwa uchi[4]

[1] 9/482.

[2] 9/483.

[3] 9/552.

[4] /552.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 28/01/2021