Salaf, wanawake na familia 6.1


1- Ibn Khallikaan amesema:

“Abu Muslim al-Khuraasaaniy alikuwa hajamiiani na wanawake kwa mwaka isipokuwa mara moja tu kwa ajili ya kusisitiza zaidi utukufu wa nafsi yake na kushughulishwa kwake na mambo ya kifalme.”[1]

2- an-Nadhwr bin ´Abdillaah amesema:

“Nilimuuliza Rawdhwah, mjakazi wa Kurz: “Ni wapi Kurz anapata ruzuku yake?” Akasema: “Alikuwa akinambia: “Ee Rawdhwah! Ukihitaji kitu basi chukua kutoka kwenye shimo hili.” Nilikuwa nikichukua kila ninachokihitaji.”[2]

3- Abu Haazim amesema:

“Mtu aliye na tabia mbaya anaisibu nafsi yake mwenyewe zaidi. Hakika yeye mwenyewe ni mtihani juu ya nafsi yake. Kisha mke wake, kisha watoto wake. Anaingia nyumbani wakiwa wako katika furaha. Tahamaki tu wanaposikia sauti yake basi wanakimbia mbali naye. Mpaka mnyama wake anayempanda anakimbia kwa sababu anamrushia mawe. Mpaka mbwa wake anaruka juu ya ukuta pindi anapomwona. Mpaka paka wake anakimbia mbali naye.”[3]

4- Sulaymaan bin ´Aliy, mtoto wa mfalme, ami yake na al-Mansuur. Alitawala Baswrah kwa kipindi fulani. Imepokelewa namna ambavyo siku moja alikuwa katika paa la jumba la kifalme na akawasikia wanawake wakisema:

“Laiti mtoto wa mfalme atatuona akatutajirisha.”

Hivyo akawarushia johari na dhahabu[4].

5- Ibn Sa´d amesema:

“Sulaymaan at-Taymiy yeye na mwanae walikuwa wakiizunguka misikiti usiku na wakiswali katika msikiti mmoja kisha wanaenda katika msikiti mwingine, mpaka kunachomoza alfajiri.”[5]

6- Yuunus bin ´Ubayd amesema:

“Yahifadhi mambo haya matatu kutoka kwangu: Asiende mmoja wenu kwa mfalme kwa ajii ya kumsomea Qur-aan, asikae chemba mmoja wenu na mwanamke kwa ajili ya kumsomea Qur-aan na mmoja wenu asiwasikilize Ahl-ul-Ahwaa´.”[6]

7- Kahmas alikuwa ni mwenye kumtendea wema sana mama yake. Mama yake alipofariki ndio akaenda kuhiji kwa mara ya kwanza na akabaki Makkah mpaka alipofariki.”[7]

8- Jariyr adh-Dhahabiy amesema:

“Ibn Jurayj alikuwa akionelea kuwa Mut´ah inafaa[8] na hivyo akaoa wanawake 60. Inasemekana kwamba aliwataja wote kwa majina yao mbele ya watoto wake ili asije yeyote akawaoa baada ya baba yao kufanya nao Mut´ah.”[9]

9- Hammaad bin Zayd amesema:

“Kuna bwana mmoja alikuwa anamlalamikia Yuunus bin ´Ubayd na kwamba anahisi njaa ambapo akasema:

“Ee mja wa Allaah! Hakika dunia hii haikustahiki. Tafuta pengine pa kwenda panapokustahiki.”[10]

10- Siku moja mama yake na Ibn ´Awn alimwita, akamwitikia kwa sauti ya juu ambapo akaacha huru watumwa wawili.”[11]

[1] 6/48.

[2] 6/85.

[3] 6/99.

[4] 6/163.

[5] 6/197.

[6] /293.

[7] 6/317.

[8] Tazama http://firqatunnajia.com/mutah-ni-umalaya/

[9] 6/317.

[10] 6/291

[11] 6/366.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 26/01/2021