Salaf, wanawake na familia 4.4


31- Imepokelewa kwamba ´Iysaa bin Mu´aawiyah amesema kuhusu Hafswah bint Siyriyn:

“Sijawahi kukutana na ambaye ni bora kuliko yeye.”[1]

Alipotajiwa al-Hasan na Ibn Siyriyn akasema:

“Mimi binafsi sioni kama kuna ambye ni bora kuliko yeye.”[2]

32- Ayyuub bin Suwayd amesimulia kutoka kwa Yuunus, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa al-Qaasim bin Muhammad ambaye amesimulia kwamba alisema kumwambia:

“Ee kijana! Naona unapupia kutafuta elimu. Je, nisikujuze juu ya chombo chake?” Akajibu: “Ndio.” Akasema: “Lazimiana na ´Amrah. Kwani alikuwa akiishi na ´Aaishah.” Nikamwendea na kuona kuwa alikuwa ni bahari isiyokauka.”[3]

33- Shu´bah amepokea kutoka kwa Abu Ma´shar ambaye naye amehadithia kutoka kwa Ibraahiym an-Nakha´iy ambaye kaeleza kwamba alikuwa akiingia nyumbani kwa ´Aaishah na akimuona amevaa kanzu nzuri. Ayyuub amesema: “Vipi alikuwa akiingia nyumbani kwake?” Akajibu:

“Alikuwa akisafiri na ami na mjomba wake kwenda hajj  akiwa ni kijana mdogo ambaye hajabaleghe. Kulikuwa na mapenzi na udugu baina yao na kulikuwa na mapenzi na udugu baina yao na ´Aaishah.”[4]

[1] 5/47.

[2] 4/507.

[3] 4/508.

[4] 4/525.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 21/01/2021