Swali: Atapokuwepo mmoja katika watu wa sasa amewazungumzia Maswahabah tunaweza kusema ya kwamba maneno yake ni kama ambavyo baadhi ya Salaf walivyowaponda baadhi ya Maswahabah. Ni vipi tutaraddi utata huu?

Jibu: Salaf ambao waliwazungumzia vibaya Maswahabah ni Khawaarij na Raafidhwah. Kuhusu Ahl-us-Sunnah hawakuwazungumzia vibaya Maswahabah. Salaf anaomaanisha ni Khawaarij na Raafidhwah. Kuhusu Ahl-us-Sunnah na Salaf walizichunga heshima za Maswahabah. ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz amesema:

“Hao ni watu ambao Allaah amezihifadhi silaha zenu kutokamana na damu zao na sisi tuihifadhi midomo yetu kutokamana na heshima zao.”

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 59
  • Imechapishwa: 29/07/2017