Salaf walikuwa hawatundiki vibao vya Aayah za Qur-aan

Swali: Ni ipi hukumu ya kutundika Aayah za Qur-aan katika chumba cha nyumbani?

Jibu: Sionelei kufanya hivyo. Kwa kuwa hili ni jambo ambalo halikufanywa na Salaf. Walikuwa hawatundiki Aayah katika majumba, kuta, gari au mipando. Walikuwa hawafanyi hili. Pengine baadhi ya watu wanafanya hivyo kama hirizi. Wanazitundika ili zihifadhi nyumba au watu wa nyumbani. Inakuwa hili limeingia katika kutundika hirizi. Haijuzu jambo hili. Mimi naonelea kuacha kufanya kitendo hichi ni bora na usalama zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/files/ls–jeddah-1430-8-20.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020