Salaf walikosea? Basi wewe sio Salafiy!


Ima useme kuwa wewe umepatia na Maswahabah walikosea au pia useme, na huu ndio ukweli, kwamba wewe umekosea na Maswahabah ndio wamepatia. Ni moja kati ya mambo hayo mawili. Ukiendelea kushikilia msimamo wako, kitu ambacho natarajia hutofanya, dogo linaloweza kusemwa ni kwamba umechanganyikiwa. Wewe unasema kuwa ni Salafiy, lakini sio Salafiy. Kimtazamo wewe ni Salafiy lakini sio Salafiy kimatendo. Kama ambavo Khatwiyb wetu hii leo ni Salafiy tofauti na khutbah yake aliyotoa hii leo. Nataraji kwamba wewe ni Salafiy, lakini kuhusiana na suala hili wewe sio mwenye kufuata mfumo wa Salaf, kwa sababu unaonelea kuwa Maswahabah walikosea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (877) Dakika: 16:37
  • Imechapishwa: 18/06/2021