Safari za utalii katika miji inayoitwa ya Kiislamu

Swali: Ni ipi hukumu ya safati za utalii katika ile miji ambayo inaitwa ni ya Kiislamu lakini ambayo imesheheni madhambi kama vile mchanganyiko na uchawi?

Jibu: Ikiwa kuna khofu kwa yule msafiri akaathirika na mambo haya, haijuzu kwake kusafiri huko. Anatakiwa kuihifadhi dini na heshima yake. Haifai kwake akasafiri kwenda huko hata kama inaitwa ni ya Kiislamu. Haifai kwake akasafiri kwenda huko ikiwa kuna machafu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 18/09/2017