Safari ya mwanamke ya mwendokasi leo


Swali: Kuhusu mwanamke kusafiri pasi na Mahram, imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba asisafiri mwendo wa mchana mmoja na usiku wake, mwendo wa siku mbili na mwendo wa siku tatu bila Mahram. Leo wakati wa safari umekuwa mfupi. Je, yanavuliwa?

Jibu: Kinachozingatiwa sio muda. Kinachozingatiwa ni ule umbali. Kinachozingatiwa ni ule umbali na sio muda hata kama safari itachukua saa moja. Hicho sio kinachozingatiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (66) http://alfawzan.af.org.sa/node/16524
  • Imechapishwa: 13/08/2017