Ama Suruuriyyah ni wafuasi wa Muhammad Suruur Zayn-ul-´Aabidiyn. Mwanzoni walikuwa wanafuata Sunnah. Walikuwa na tofauti baina yao wao na al-Ikhwaan al-Muslimuun na kadhalika baina yao wao na jumuiya ya Ihyaa´ at-Turaath. Hata hivyo lililo la ajabu na la kushangaza ni vipi wao wote wakiwemo Suufiyyah, kuwa na umoja dhidi ya Ahl-us-Sunnah. Wanaweza kadhalika kuwa na umoja na Shiy´ah dhidi ya Ahl-us-Sunnah.

Inavyoonekana ni kuwa Suruuriyyah walikuwa wanalingania katika Sunnah. Sisi na ndugu zetu tulikuwa tukisifu gazeti lao “al-Bayaan”. Yaliyowafichukua ni qadhiya ya Saddaam. Katika gazeti lao wakaanza kuwatuhumu wanachuoni kwamba hawafahamu mambo ya kisasa wakati wao wenyewe walikuwa wanamsaidia Saddaam. Maadui wa Uislamu wanafurahishwa wakati Waislamu wanaposibiwa na mambo kama haya. Wanadai kuwa wao ndio wanafahamu mambo ya kisasa. Uhakika ni kwamba ukweli umethibitika wanachuoni watukufu, kama Shaykh Ibn Baaz, Shaykh al-Albaaniy na wengineo, waliyosema ni kweli, nayo ni kwamba Saddaam – Allaah amuadhibu kwa mitihani – alitaka kuizingira Kuwait na Saudi Arabia na kuacha kundi la Ba´th waishambulie Makkah na al-Madiynah. Watu wakakabili Ba´th. Himidi zote ni za Allaah ambaye amemfedhehesha Saddaam na wasemaji wao katika al-Ikhwaan al-Muslimuun, serikali zilizomsaidia, Suruuriyyah na wengineo. Allaah amewafedhehesha na kufanya wakashindwa.

Yakafichuka mambo yao waziwazi kabisa ya kwamba ni Hizbiyyuun.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=21
  • Imechapishwa: 05/09/2020