Sababu za neema na adhabu za ndani ya kaburi

 Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Liharakisheni jeneza. Akiwa mwema, basi ni kheri mnayomtangulizia, na akiwa kinyume na hivo, basi hiyo ni shari mnayoiondoa kutoka kwenye shingo zenu.”[1]

Hadiyth inafahamisha pia kwamba neema na adhabu ya maisha ya ndani ya kaburi zinatokana na sababu. Neema za maisha ya ndani ya kaburi ni wema, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Akiwa mwema… “

Wema ni lililo lililokusanya kumsadikisha Allaah na Mtume Wake pamoja na kumtii Yeye na Mtume Wake. Kwa msemo mwingine inahusiana na kusadikisha maelezo, kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo.

Adhabu ya maisha ya ndani ya kaburi ni kule kufanya mapungufu katika wema. Inaweze kuhusiana na kutilia shaka dini, kutumbukia katika mambo ya haramu au kuacha kitu katika mambo ya wajibu na ya faradhi. Sababu zote zilizopambanuliwa katika Hadiyth na mapokezi zinarejea katika hayo. Ndio maana Allaah akasema:

لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ

“Hatouingia kuchomeka isipokuwa muovu mkubwa, ambaye amekadhibisha na akakengeukia mbali.”[2]

Wameyakadhibisha maelezo na wakayapa mgongo maamrisho.

[1] al-Bukhaariy (1315) na Muslim (944).

[2] 92:15-16

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjat-ul-Abraar, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 01/03/2021