Swali 132: Je, ni kweli kwamba wanawake ndio wakazi wengi wa Motoni? Kwa nini iwe hivo?

Jibu: Ni kweli. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaambia wakati alipokuwa anawatolea Khutbah:

“Enyi kongamano la wanawake! Toeni swadaqah. Kwani hakika mimi nyinyi ndio wakazi wengi wa Motoni.”

Kumepokelewa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) utatizi huu ulioulizwa na muulizaji: “Tukasema: “Kwa nini, ee Mtume wa Allaah?” Akasema:

“Mnakithirisha laana na mnakufuru wema.”

Akasababisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sababu ya kuwa kwao wengi Motoni. Kwa sababu wanakithirisha laana, matusi na maapizo na wanakufuru wema ambao ni yule mume. Ndio maana wakawa wakazi wengi wa Motoni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 533
  • Imechapishwa: 14/08/2019