Sababu ya Salaf kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Kitendo cha Salaf kuwakimbiza watu mbali na Ahl-ul-Bid´ah, kutahadharisha nao, kutokaa nao na kutowasikiliza ilikuwa ni kwa sababu ya kuwakimbiza watu mbali nao au ilikuwa ni kwa sababu ya kuogopa wasiingie ndani ya waliyoingia wao?

Jibu: Ilikuwa ni kwa sababu ya kuwakimbiza watu mbali nao na wasitumbukie ndani ya yale waliyoingia wao. Kwa msemo mwingine watu wawakimbie mbali ili wajirejee na watubu. Aidha yule mwenye kukaa nao asitumbukie katika yale waliyoingia wao.

Swali: Vipi kuwalingania?

Jibu: Ni vizuri. Ni katika kulingania kwa Allaah. Ni jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22897/لماذا-نفر-السلف-من-اهل-البدع-وحذروا-منهم
  • Imechapishwa: 14/09/2023