Sababu ya kuthibiti maandiko mengi juu ya kufufuliwa

´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) anasema kuwa miili kufufuliwa ni kitu wameafikiana juu yake waislamu, mayahudi na manaswara. Anasema Jalaal ad-Dawaaniy ya kwamba ni maafikiano ya dini zote na ni jambo limetolewa ushahidi na maandiko ya Qur-aan.

Maandiko ya kufufuliwa ni mengi zaidi kuliko maandiko juu ya sifa na majina ya Allaah. Kuzungumziwa juu ya kufufuliwa katika Qur-aan ni kwingi zaidi kuliko kuzungumziwa juu ya Mola. Hilo ni kwa sababu ya wingi wa makanusho ya kufufuliwa na uchache wa makanusho ya Mola. Hilo ni kutokana na kwamba Mitume wote (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) maneno yao ni yenye kuafikiana juu ya kumuamini Allaah. Kumkubali Mola ni kitu cha kimaumbile kilichoenea kwa wanaadamu. Wanaadamu wote kimaumbile wanamkubali Mola isipokuwa yule mwenye kufanya jeuri tu kama Fir´awn. Tofauti na imani ya kuamini siku ya mwisho ambayo inakanushwa na watu wengi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (02/639)
  • Imechapishwa: 19/05/2020