Sababu ya kuenea jezi za maklabu ya mpira katika jamii zetu

Swali: Tunaomba nasaha juu ya watoto wa kiume ambao wanavaa mavazi ya mazoezi yaliyoandikwa juu yake majina ya makafiri katika wachezaji na wengineo?

Jibu: Hili linarudi katika ule msingi wa malezi. Kuna mambo mawili muhimu katika malezi:

1 – Mtu, pasi na kujali umri wake, kama atakuwa na miaka 60 na amezowea tabia fulani na kuikariri – ni mamoja tabia hiyo ni mbaya au nzuri – basi analazimiana nayo. Hali inakuwa hivo mpaka katika kipindi cha mwisho wa maisha yake wakati roho inatolewa kutoka katika mwili wake. Mtu akiizoweza nafsi yake na tabia nzuri au sifa mbaya basi tabia hiyo inakuwa ni sehemu ya maisha yake. Tumewaona watu wakati wa kukata roho wanaimba nyimbo walizokuwa wanazikariri katika maisha yao. Baadhi yao wanatamkishwa shahaadah lakini wanakariri waliyokuwa wamezowea kufanya katika matendo mabaya.

2 – Kuna watu katika kipindi chao cha mwisho cha kutolewa roho wameonekana wakisoma Qur-aan na umri wao unazidi miaka 100.

Ninachotaka kusema ni kwamba tumeghafilika upande wa kuzilea nafsi zetu na upande wa kuwalea watoto wetu. Mshairi anasema:

Hukulia mtoto chipukizi kati yetu

juu ya kile alichokuwa amemzoeza baba yake

Baba yake akimzoweza juu ya tabia nzuri huizowea na akimzoweza juu ya tabia mbaya huizowea na tabia hiyo inakuwa ni sehemu katika maisha yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-10/lqa-mftoh-godian.mp3
  • Imechapishwa: 12/09/2022