Swali: Je, mtu asujudu Sujuud-us-Sahuw kwa kule kuwa na shaka katika Swalah yake?

Jibu: Ndio. Hii ni sababu miongoni mwa sababu za Sujuud-us-Sahuw. Sababu za Sujuud-us-Sahuw ni tatu:

1- Kuzidisha katika Swalah (az-Ziyaadah).

2- Kupunguza katika Swalah (an-Naqs).

3- Kutilia shaka kwa jumla (ash-Shakk).

Akitilia shaka juu ya idadi ya Rakaa alizoswali, akitilia nguvu kitu basi atatendea kazi kile ambacho dhana yake imeegemea zaidi na asujudu Sujuud-us-Sahuw. Lau dhana yake haikuegemea zaidi mahala popote, bi maana isimbainikie kwake moja kati ya mambo mawili, basi ajengee juu ya yakini, yaani atachukua idadi ile ndogo na akamilishe Swalah yake kisha atasujudu Sujuud-us-Sahuw.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-8-5.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014


Takwimu
  • 305
  • 373
  • 1,819,073