Sababu kubwa ya kuitikiwa du´aa

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

10- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swallla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) ni Mwema na anakubali kilicho chema tu. Allaah (Ta´ala) amewaamrisha yale aliyowaamrisha Mitume, akasema (Ta´ala):

“Enyi Mitume! Kuleni katika vitu vyema na mfanye mazuri.” (23:51)

Amesema (Ta´ala):

” Enyi mlioamini! Kuleni katika vitu vyema ambavyo tumekuruzukuni.” (02:172)

Kisha akataja kuhusu mtu aliyesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni akisema: “Ee Mola! Ee Mola! Wakati chakula chake cha haramu, kinywaji chake ni cha haramu, kivazi chake ni cha haramu na anashibishwa na haramu. Vipi basi atajibiwa?”

Hadiyth hii ni dalili inayoonyesha ya kwamba kutumia chakula chema [kilichotakasika na haramu] ni miongoni mwa sababu kubwa za kupokelewa du´aa na kwamba mtu akienda kinyume na sababu hii, hata kama kutapatikana sababu nyinginezo, mara nyingi du´aa haiitikiwi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Vipi basi atajibiwa”?

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 198
  • Imechapishwa: 16/05/2020