Saa ya kwanza ijumaa


Swali: Ni lini mtu anaweza kuanza kwenda katika swalah ya ijumaa? Je, ni moja kwa moja baada ya swalah ya Fajr ili mtu aweze kulipwa kuwa amefika katika ile saa ya kwanza?

Jibu: Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa ile saa ya kwanza inaanza moja kwa moja baada ya swalah ya Fajr. Wengine wakasema ni baada ya jua kuchomoza. Hii ndio niliyosikia ikichaguliwa na Shaykh Ibn Baaz, ya kwamba ni baada ya jua kuchomoza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/de
  • Imechapishwa: 30/09/2017