Swali: Ni ipi hukumu ya rushwa ikiwa haki yangu ni yenye kujulikana au kiwango changu hakitotimia isipokuwa kwa njia hiyo?

Jibu: Rushwa haijuzu kwa sababu maana yake ni kusaidia katika batili, kusaidia kupoteza haki na kuwadhulumu watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemlaani mtoaji rushwa na mpokeaji rushwa.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… na muunganishi.”

Bi maana pia yule anayekaa katikati ya wawili hao.

Haijuzu kusaidiana katika batili na dhambi. Aitafute haki yake kutoka katika njia iliyowekwa katika Shari´ah. Ikiwa kuna mtu anayemzuia haki yake basi amshtaki na amfichukue kwa kuchukua kwake usahali. Asimsaidie juu ya kumuasi Allaah kwa rushwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3662/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D8%AF%D9%81%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%B4%D9%88%D8%A9-%D9%84%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D8%B9%D8%A7%D8%AF%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D9%82%D9%88%D9%82
  • Imechapishwa: 19/02/2020